JINSI YA KUFICHA FILE LAKO LA KWENYE COMPUTER ILI LISIONEKANE NA WENGINE BILA KUTUMIA SOFTWARE YOYOTE
Karibu tena ndugu msomaji wa blog yako ya Mbinda Technologies, Katika mfululizo wa makala zetu leo hii nakuletea makala itakayokupa ujuzi wa namna ya kuficha file lako la computer ili watu wengine wasilione.
Njia hii itakuwezesha kuficha file lako pasipo kutumia software yoyote ile. Cha msingi fuata hatua zifuatazo.
1: Tengeneza file / folder jipya kwenye computer yako kwa kubonyeza right click => Folder => New. kama hivi:-
2:Kisha baada ya hapo futa jina la file lako mpya kwa kubonyeza key ya F2 kisha delete Kisha shikilia Alt key na uandike 255 kwa kutumia keyboard za namba zile za pembeni tu kama hauna hii njia haitafanya kazi kwako. kama hivi:-
3: Kisha baada ya hapo bonyeza right click => properties. kama hivi:-
4: Kisha baada ya hapo chagua customize => change icon. kama hivi:-
5: Kisha baada ya hapo chagua mpaka sehemu iliyo haina kitu kisha ukiipata bonyeza hapo kama hivi:-
6: Kisha baada ya hapo bonyeza OK. kama hivi:-
7: Kisha Baada ya hapo Bonyeza APPLY => OK. kama hivi:-
8: Kisha baada ya hapo file lako halitaonekana kiurahisi bali litaonekana kwa umbali kama umbo la mstatili. Na hapo utakua umeshalificha file lako kama hivi:-
********** MWISHO **********
KWA MAONI NA USHAURI TAFADHALI USISITE KUTUTAFUTA KWA NAMBA 0767973853 Whatsapp / Telegram / sms / call au unaweza kutuandikia barua pepe kwendambinda74@gmail.com
AHSANTE!
== ADVERTISEMENT ==
TUNAPOKEA MATANGAZO YA BIASHARA MBALIMBALI NA KUYATANGAZA KATIKA KURASA ZETU ZINAZOSOMWA KWA WINGI HAPA NCHINI, TANGAZA BIASHARA YAKO LEO KWA BEI NAFUU KABISA YA Tsh 5000/= KWA WIKI. KWA MAWASILIANO TUPIGIE / SMS 0767973853 / mbinda74@gmail.com
No comments