WHATSAPP TRICK LECTURE 1: JIFUNZE NAMNA YA KUTUMIA WHATSAPP KWENYE COMPUTER YAKO BILA KUTUMIA SOFTWARE YOYOTE
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
Karibu ndugu mpenzi msomaji wa makala zetu, Siko ya leo katika mfululizo wa makala zetu za Technology, Mbinda technologies leo tunakuletea Trick (mbinu) mpya ya kutumia mtandao wa whatsapp kwenye laptop au computer yako, Mbinu hii itakusaidia kuweza kutumia mtandao wa whatsapp ukiwa na computer yako hata kama simu yako umeiacha nyumbani au mkoani au uwapo nje ya nchi na simu yako umeiacha ndani ya nchi.
FAIDA YA MBINU HII
1: Utaweza kutumia whatsapp kwenye computer yako hata kama simu umeiacha mbali sana kama vile nyumbani, ofisini au nje ya nchi.
2: Itarahisisha kazi ya kuandika message ndefu sana kwa sababu utakua unatumia keyboard za computer yako
3: Utaweza kushare document, Picha, Audio au Video zilizopo katika computer yako kirahisi kabisa
Hizo ni baadhi ya faida tu za kutumia whatsapp kwenye computer yako
Pia hii njia ina baadhi ya changamoto kama vile
1: Mbinu hii inahitaji internet connection ya kwenye simu yako na pia kwenye computer yako
2: Mbinu hii inahitaji umakini sana kwani mtu naweza akaunganisha accout yako ya wahtsapp kwenye computer yako na akaweza kusoma sms zako na pia kupost mambo mabaya kwa kutumia account yako.
HATUA KWA HATUA JINSI YA KUTUMIA WHATSAPP KWENYE COMPUTER / LAPTOP YAKO.
MAHITAJI
1: SIMU YAKO YA MKONONI (SMARTPHONE)
2: COMPUTER YAKO
4: internet connection kwenye computer na simu yako
FUATA HATUA ZIFUATAZO
1: ingia kwenye opera mini yako na kisha tafuta mahala palipoandikwa extension kama inavyoonekana hapa
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
2: Baada hapo bonyeza mahala palipoandikwa Get more extension
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
3: Kisha baada ya hapo kitakuja kibox cha kutafuta (search box) na uandike whatsapp web na uchague whatsapp web ya kwanza kushoto kama hivi
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
3: Kisha baada ya kubonyeza hapo kwenye hiyo whatsapp ikifunguka bonyeza kitufe cha kilichoandikwa ADD TO OPERA kama hivi
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
4: Kisha baada ya hapo bonyeza nembo ya whatsapp ambayo itakia juu kabisa upande wa kulia kama hivi
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
5: Baada ya kubonyeza hiyo nembo itafunguka , hapo unatakiwa kuweka alama ya Tick kwenye option ya KEEP CONNECTED kama hivi
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
KISHA BAADA YA KUFUNGUKA HIVYO ACHA COMPUTER YAKO HIVYO HIVYO WALA USIFUNGE INTERNET CONNECTION
6: Sasa chukua simu yako na ufungue application ya WHATSAPP kisha ubonyeze vidoti vitatu vilivyopo juu kabisa ya whatsapp yako na kisha chagua WHATSAPP WEB kama hivi
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
7: Kisha baada ya kubonyeza whatsapp web itakuja option inayokuelekeza namna ya kuunganisha whatsapp ya simu yako na computer hapo utatakiwa ubonyeze maandishi yalioandikwa OK, I GOT IT kama hivi
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
8: Baada ya hapo utatakiwa uielekeze camera ya simu yako kwenye ule mchoro (QR code) uliopo kwenye computer kama huu hapa chini
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
9: Tulia kidogo wakati umeielekeza camera ya simu yako kwenye huo mchoro mpaka mchoro huo uondoke (mara nyingi simu ikimaliza kuscan huo mchoro hutoa vibration fulani hivi) kisha baada ya hapo itasearch kidogo na baada ya mda mfupi utaona chatting zako zote zipo kwenye computer yako kama hivi
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
10: kama ukiizima computer yako au search engine yako basi ili kutumia whatsapp tena hautakiwi kuscan ile picha tena unachotakiwa kufanya ni kubonyeza kapicha (icon) ya whatsapp iliopo juu kabisa ya operamini yako kama hivi
![]() |
http://mbindatechnologiestz1.blogspot.com |
***************** MWISHO *******************
KWENYE SOMO LIJALO TUTANGALIA NAMNA YA KUTUMIA WHATSAPP KWENYE GOOGLE CHROME, HII NI KWA WALE AMBAO WANAPENDELEA KUTUMIA GOOGLE CHROME ENDELEA KUTEMBELEA Mbinda Technologies kwa ujuzi zaidi bonyeza hapa ili kujua mengi 

KWA MAONI NA USHAURI TUANDIKIE KUPITIA WHATSAPP / TELEGRAM / SMS KWENDA 0767973853 PIA BARUA PEPE (E - MAIL) mbinda74@gmail.com
PIA KWA MAHITAJI YA KUFUNGULIWA BLOG YA KIJANJA NA KISASA ZAIDI KWA GHARAMA YA Tsh 15000/=, NA TUNATOA PIA HUDUMA YA DOMAIN NAME REGISTRATION YAANI KUBADILISHA BLOG ZENYE
_ _.blogspot.com NA KUWA _ _.com KWA Tsh 25000/= tu KWA MWAKA MZIMA, PIA KWA MAHITAJI YA LOGO MBALIMBALI WASILIANA NASI KWA WHATSAPP / TELEGRAM / SMS KWA NAMBA 0767973853 PIA BARUA PEPE (E - MAIL) mbinda74@gmail.com
PIA TUNAPOKEA ODA ZA HUDUMA HIZO
AHSANTE
Tupo pamoja mkuuu
ReplyDeletethanks good
ReplyDelete