• Breaking News

    YOUTUBE CHANNEL LECTURE 2: JIFUNZE JINSI YA KUWEKA KU UPLOAD VIDEO KWENYE CHANNEL YA YOUTUBE


    Karibu tena ndugu msomaji wa blog yako pendwa ya Mbinda Technologies.

    Jana tulizungumzia jinsi ya kufungua / kuanzisha channel ya youtube, basi leo tutaangalia namna ya kuweka video katika channel ya youtube, kwa hiyo nakusihi kuwa makini na hatua zitakazo elezewa ili uweze kufanya practical hii peke yako.

    FUATA HATUA ZIFUATAZO 
    1:Ingia youtube kisha sign in kwa kutumia ile e mail ambayo ulitengenezea channel kisha baada ya hapo chagua chaguo la my channel => chagua kitufe cha ku upload kipo juu upande wa kulia, kama hivi:-


    2: Baada ya hapo bonyeza sehemu palipoandikwa select files to upload, kama hivi:-


    3: Kisha baada ya hapo utakua directed moja kwa moja mpaka kwenye mafile yako unachotakiwa kufanya ni kuchagua video yako unayohitaji ku upload => open kama hivi:-


    4: Baada ya hapo video yako itaanz akuingia taratibu, hapo utatakiwa kuwa mvumilivu tu na ikishakua tayari itakuletea vibox vingi tu, unachotakiwa kuchagua ni kama viwili tu ambapo cha kwanza utaandika jina la video yako na cha pili utaandika maelezo machache kuhusiana na video yako => bonyeza kitufe cha finish . kama hivi:-

    Mpaka hapo video yako itakua online tayari kwenye channel yako ya youtube hivyo unaweza ukashare na marafiki / wadau.

    usikose lecture ya kesho ambayo itahusu jinsi ya kuunganisha channel yako youtube na matangazo ya google ili ulipwe pesa.

    **********   MWISHO  **********


    KWA MAONI NA USHAURI WEKA KWENYE KIBOX CHA MAONI HAPO CHINI AU TUTUMIE KWA WHATSAPP/Telegram/SMS kwenda 0767973852 / barua pepe kwenda mbinda74@gmail.com
     
    AHSANTE
       

         

    No comments