Mafunzo ya Blog Sehemu ya Nne: MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLYA YA KUANZISHA BLOG
Habari wapenzi wasomaji wa blog ya Mbinda Technologies Leo nimeona nizungumze na Watu wanaotaka kuanzisha BLOG
MAANA YA BLOG
BLOG ni website ndogo ambayo hutumiwa kwa taarifa mbalimbali kama MICHEZO,HABARI,MZIKI,FASHION na mengine mengi..Tofauti iliyopo kati ya blog na WEBSITE ni kuwa BLOG mara nyingi ina "Limited Pages" nikiwa na maana kuwa ina idadi maalum za kurasa na HAIHITAJI UWE NA DATABASE
FAIDA ZA KUWA NA BLOG
Blog mara nyingi ziko HOSTED (zimewekezwa / zinasimamiwa) na BLOGGER au WORDPRESS ambao hutoa huduma hii BUREEEE.Ninacho maanisha ni kuwa HAKUNA MALIPO YOYOTE
Kwa mantiki hii,BLOG imekuwa kitega uchumi kizuri hasa kwa nchi zinazoendelea na baadhi ya nchi kama NIGERIA.Wanatengeneza hela nzuri sana kiasi kwamba mtu anafikia hatua ya kutoona haja ya KUAJILIWA TENA.
MAMBO MATATU YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BLOG
Kabla hujaanzisha blog yoyote,ni lazima ukae chini ujiulize LENGO la kuwa na blog ni nini!!!!. Usianzishe blog kwa kuwa tu wengine wana blog pia.,HAPANA,utakuwa unapoteza muda na pengine ni bora ukafanya mambo mengine ya msingi zaidi.Yafuatayo ni mambo makuu matano yakuzingatia
1. FIKIRIA NAMNA YA KUWATEKA WASOMAJI
Kitu cha kwanza kabisa ni lazima ufikirie juu ya wasomaji..Jiulize ni nani ataeyeitembelea BLOG yako.kwa kufanya hivyo itakusaidia kujua na kupanga juu ya habari za kuweka katika BLOG yako.Ifanye blog yako iwe na MUONEKANO MZURI,kiasi kwamba mtu akiitembelea siku moja atatamani na kesho arudi tena hata kama huna habari nzuri ulizoandika.
2. NI VIZURI KILA HABARI IKAWA NA PICHA.
Picha hubeba ujumbe mkubwa sana mana ni kielelezo tosha kabisa cha taarifa unayozungumzia. Huwezi ukasema kwa mfano " mpekuzi akutwa baa" bila kuwa hata na picha moja inayothibitisha kuwa ni kweli mpekuzi amenaswa baa!! .Wafanye wasomaji wako wakuamini.Lakini pia ni lazima picha yako iwe na muonekano mzuri
3. JITAHIDI BLOG YAKO IWE NA MUONEKANO MZURI
Hapo mwanzo nilisema kuwa HUDUMA YA KUWEKEZA BLOG NI BURE. Ni kweli kabisa lakini kuna gharama ndogo wakati wa utengenezaji wake.Ninacho maanisha ni kuwa,ni lazima umtafute mtu mwenye ujuzi wa HTML na JAVASCRIPT ili akutengenezee blog yenye " interface nzuri".Vinginevyo utaishia kuwa na blog ambayo haina wasomaji.Gharama ya kuanzisha na kutengeneza blog inategemea na mtu mwenyewe.Hakuna bei maalum.Kama utaridhia toka moyoni kuwa unataka kuwa na blog,basi usihangaike.MIMI PIA NI MJUZI NA MTAALAM WA KUTENGENEZA BLOGS NA WEBSITE. Kwa kuwa lengo langu ni kuwaelimisha wenzangu ili nao wanufaike na huduma hii,basi,ntakufanyia bei ya kubinadamu sana ambayo najua huwezi amini.Lengo langu ni kukusaidia na si kukuumiza
Kama unaswali lolote juu ya BLOGS ,naomba uandike maoni yako hapo chini nami ntakujibu na kukuelimisha zaidi.Na kama umeguswa na MAADA hii na hivyo umepanga kuanzisha blog,basi usiste kuwasiliana na mimi.kama nilivyokuahidi,lengo langu ni kukusaidia na si kukuumiza.
Niandikie sms : 0767973853 au nitumie email: mbinda74@gmail.com
ANGALIZO: Kama una swali,naomba uniulize kwa njia ya maoni hapo chini badala ya kuniandikia sms au email
Nimeyapenda sana mafundisho YAKO, na ginsi unavyo jitowa kwajili yetu. Ila na Mimi naitaji kuwa na Blog Yangu kwajili ya Photography na Designer. Ningependa unisaidie pia unitengenezee ya kwangu. My contact +255655011175
ReplyDelete