Thursday, May 8.
• Breaking News

ADVANCED BLOG DESIGN LECTURE 4: JIFUNZE NAMNA YA KUZIFANYA LABEL (LEBO) ZAKO ZIFANYE KAZI NA JINSI YA KUZITUMIA

Habarini za wakati huu tena wapenzi wasomaji wa makala hizi, Ni matumaini yangu wote ni wazima wa afya na mnaendelea vema na majukumu nyenu ya kulijenga Taifa.

Jana tuliangalia maana ya lebel (lebo) na jinsi ya kutengeneza na kuiweka katika blog pages, basi leo tutaangalia jinsi ya kuziamusha (ku activate) labels zetu ili ziweze kutumika katika kurahisisha upatikanaji wa habari au makala fulani ndani ya blog yako

FUATA HATUA ZIFUATAZO ILI KUAMUSHA (KU ACTIVATE) LABELS ZAKO NA KUZITUMIA

1: SIGN IN KWENYE BLOGGER

2: KWENYE DASHBOARD YA BLOG YAKO CHAGUA / SELECT THEME / TEMPLATE kiaha chagua EDIT HTML

3: Baada ya hapo ukishachagua EDIT HTML itakuja window hii

4: Hapo sasa ndio penyewe sasa utakachotakiwa kufanya ni kubonyeza keyboard zifuatazo za computer yako (Ctrl + F) Hii inatusaidia kuweza kusearch keyword (neno husika tu).  baada ya hapo itakuja hivi

5:  Katika kisanduku hicho cha kutafuta (search box) andika key word yoyote iliopo katika labels zako za zamani mfano angalia hapo chini

6: Baada ya kukariri label yako basi rudi kwenye uwanja wa CODE  na kuandika ile label yako kwenye kisanduku cha kutafuta (search box) kisha bonyeza kitufe cha ENTER kwenye keyboard yako na itakuleta moja kwa moja kwenye CODE za lebels kama hivi;

Kumbuka hatua hii si lazima lakini ni muhimumkwa sababu inatupeleka kwenye code husika mija kwa moja hivyo kuokoa muda pia kama wewe ni mtaalamu wa code basi utashuka chini             (scroll down ) mpaka uzikute code hizo

ANGALLIZO KWA WALE AMBAO HAWAJAWAHI KUBADILISHA LABEL TANGU WABADILISHE TEMPLATES BASI NYIE BAADA YA KUBONYEZA ENTER KEY ITAKUJA WINDOW YA HIHI AMBAYO NI TOFAUTI KIDOGO NA HIYO YA CHINI,angalia picha hii

7: Hatua hii inataka umakini sana, Baada ya kuja window hiyo hapo chini unachotakiwa kufanya ni kufuta hiyo alama ya RELI (#) TU  kuandika link ya blog yako mahali ulipofuta hiyo reli ukianza na http-----. mfano wa label yangu ile ya NGURUWE itakuwa hivi ==>
NGURUWE (PIGS)
kumbuka maneno ya mwanzo na mwisho mfano (href=' '>
) huwa yanakuwapo automatic so usijichangaye wewe unatakiwa ujaze nafasi zilizo wazi kama inavyoonekana kwenye picha hii hapa chini

KWENYE VIBOX VYA KWANZA YAANI HUMU KATIKATI UNAJAZA VIFUATAVYO:-

I. Anwani / link ya blog yako mfano:- http://christophambinda.blogspot.com
II. Bila kuacha nafasi utaandika hivi baada ya link ya blog yako:- /search/label/NGURUWE (PIGS)

KWENYE VIBOX VYA PILI YAANI VILE VILIVYO UPANDE WA KUSHOTO UNAJAZA LABEL YAKO SASA YA KUDISPLAY. Mfano:- NGURUWE (PIGS)

TUKIUNGANISHA KWA PAMOJA SEHEMU HIZI ZA SENTENSI NDIO TUNAPATA LEBO YETU, BAADA YA KUUNGANISHA SENTENSI (CODE)YETU ITAKUA KAMA HIVI:-

href='http://christophambinda.blogspot.com/search/label/NGURUWE (PIGS)'>NGURUWE (PIGS)

KWA HIYO TENGENEZA LABEL ZAKO ZINAZOFUATA KWA MFUMO HUU

BAADA YA KUMALIZA KUTENGENEZA LEBO TOFAUTI TOFAUTI BONYEZA SAVE CHANGES KAMA INAVYOONEKANA KATIKA PICHA HAPO CHINI;

SASA TUJIFUNZE NAMNA YA KUWEKEA LABEL KWENYE POST ZETU

FUATA HATUA ZIFUATAZO:-

1: FUNGUA UWANJA WAKO WA POST

2: UKISHAMALIZA KUANDIKA POST YAKO BONYEZA KWENYE SEHEMU PALIPOANDIKWA LABELS PAPO UPANDE WA KUSHOTO WA KOMPUTER YAKO KAMA  INAVYOONEKANA KWENYE PICHA;

HAPO ANDIKA JINA LA LEBO YAKO KAMA ULIVYOONDIKA KULE KWENYE CODES MFANO SISI TULITUMIA LEBO YA NGURUWE (PIGS)  SO NA HAPA UTATAKIWA UANDIKE NGURUWE (PIGS) PASIPO KUACHA NENO LOLOTE LILE WALA KUOGEZA

PIA POST MOJA INAWEZA IKAWA NA LABELS ZAIDI YA MOJA, SASA ILI KUWEKA LEBO ZAIDI YA MOJA KWENYE POST MOJA FANYA YAFUATAYO

UKIMALIZA KUANDIKA LEBO YA KWANZA UNATAKIWA UWEKE ALAMA YA MKATO NDIO UWEKE LEBEL NYINGINE. ANGALIA PICHA HII;

***** SOMO LETU LA LEO LINAISHIA HAPO *****

TUKUTANE TENA KESHO KWENYE SOMO AMBALO TUTAJIFUNZA NAMNA YA KUONDOA FOOTER CREDIT KATIKA TEMPLATE ZETU AMBAZO TUMEZIWEKA KWA HIYO USIKOSE SOMO LIJALO

KWA MAONI NA USHAURI TUANDIKIE KWENYE KISANDUKU CHA MAONI AU NIULIZE KUPITIA WHATSAPP / TELEGRAM KWA NAMBA 0767973853 AU  E - MAIL mbinda74@gmail.com  PIA UNAWEZA NIPIGIA SIMU YA MKONONI KWA MSAADA ZAIDI

AHSANTENI.

1 comment:

1. Mambo? mm naswali.je kama leber yenyewe ina ruka kanafasi na umesema nsilike nafasi niiandikaje?/

ReplyDelete