ADVANCED BLOG DESIGN LECTURE 2: Jifunze namna ya kubadili muonekano (Template) kwenye blog yako

LEO TUTAENDA KUJIFUNZA NAMNA YA KUBADILISHA TEMPLATE (muonekano) YA BLOG
HATUA ZA KUFUATA
1: Fungua web browser yako kisha search au Bonyeza hapa (www.mbindatechnologiestz1.blogspot.com)

2: Kisha baada ya hapo anza kutafuta post zilizoandikwa free blog template


3: Hapo utatakiwa kuchagua template unayoitaka kisha ifungue

4: Mara baada ya kuifungua utatakiwa ubonyeze mahala palipoandikwa DEMO ili kuiangalia
template yako vema.

5: Kama umeridhiswa na template hiyo rudi nyuma kisha bonyeza mahala palipoandikwa
"DOWNLOAD"

6: Mara baada ya kudownload nenda kwenye computer yako upande wa desktop kisha bonyeza
file la my computer

7: Baada ya hapo fungua file la DOWNLOAD kwenye Computer yako

8: Baada ya hapo tafuta jina la Template yako ulio idownload kisha ifungue kwa kuibonyeza mara
mbili

9: ikifunguka sasa tafuta file lililo na mwisho huu ( .xml) kumbuka unaweza kutumia software yoyote ku unzip file mfano mimi natumia win rar

10: kisha licopy na uliweke kwenye desktop

11: Rudi tena kwenye web browser yako kisha log in kwenye blogger kisha ifungue dashboard
ya blog yako

12: Baada ya hapo shuka mpaka chini palipoandikwa Theme / template na ufungue

13: Kisha uchague kitufe cha BACKUP / RESTORE kipo juu kule kabisa

14: Baada ya hapo itakuja window yenye option tatu unachotakiwa kufanya ni kubonyeza maandishi
yalioandikwa CHOOSE FILE

15: Baada ya hapo itakuja window ya kuchagua mafile unachotakiwa kufanya ni kuchagua location sahii ya template yako mfano sisi tuliiweka kwenye deskitop so utachagua file lako lile linaloishia na (.xml)


16: Baada ya hapo upload file lako na kisha save changes

HAPO UTAKUA UMEKWISHA KUBADILI TEMPLATE YA BLOG YAKO ILI KUHAKIKISHA
BONYEZA KITUFE CHA VIEW MY BLOG ILI KUONA TEMPLATE MPYA YA BLOG YAKO

AHSANTE TUKUTANE LECTURE IJAYO
Lecture ijayo itahusu jinsi ya kuedit template yetu ili kuondoa baadhi ya vitu tusivyo vitaka.
REMEMBER: PRACTISE MAKE PERFECT
No comments